Jumapili, 1 Desemba 2013

PAUL WALKER AFARIKI DUNIA

Msanii muigizaji wa marekani PAUL WALKER amefariki dunia masaa machache yaliyo pita huko katika jiji la LOS ANGLE nchini marekani baada ya ajili mbaya waliyo ipata.

Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi walio kua nao wakati walipo kua wakirejea nyumbani baada ya kutoka katka part.
Paul Walker na mwenzake walikua wakirejea nyumbani na gari yao ambayo alikua akiendesha rafiki yake ambaye nae inasemekan pia ni dereva mzuri sana.
Wakati wakiwa njiani ndio walipo gonga taa ya barabarani na kwenda kugonga mti ulio kua pembeni,na kusababisha gari yao kubinuka vibaya mpaka tairi za gari hiyo zilibasti na kuanza kuwaka moto na kuteketea vibaya.

Paul walker ambae walikua katika maandalizi ya kutoa mwendelezo wa filamu yao ya FAST&FURIOUS 7.
Inasemekana kwamba tutaweza kumuona tena kwa mara nyingine katika filamu hiyo ambayo itatoka hiv karibuni,kwani Paul tayari amesha kamilisha baadhi ya vipande vyake vya kuigiza.

PAUL WALKER amefariki akiw na umri wa miaka 40 ameacha mke na mtoto mmoja wa kike mwenye umri wa miaka 12.

Ametuachia mashabiki wake huzuni kubwa sana ndani ya nyoyo zetu kwani tulimpenda sana ila mumgu alimpend zaidi.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU PAUL WALKER MAHALA PEMA PEPONI AMEEN

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni