Jumanne, 8 Aprili 2014

NGASA AMZAWADIA WEMA MPIRA WA HATITRICK.....!!

Mchezaji wa timu ya Soka ya Yanga Mrisho Khalfani Ngasa alifanikiwa kufunga (hatrick)mabao matatu katika mechi dhidi ya Jkt Ruvu,lakini ametoa kauli kwa kusema kuwa mpira alio kabidhiwa kwa kufunga mabao hayo anampelekea shemeji yake Wema Sepetu.Akizungumza baada ya mechi hiyo ya ligi kuu Tanzania Bara iliyo malizika kwa timu yake kushinda jumla ya mabao 5-1 Ngasa huku akionyesha kuwa na furaha,alisema kuwa mpira huo umeongeza hamasa kwa timu yake;lakini moja kwa moja atampelekea Wema ambaye ni mpenzi Wa Msanii Diamond. "Mashabiki hawatakiwi kukata tamaa ba timu yao,sisi tunapigana mpaka dk ya Mwisho ilikuhakisha tunashinda mechi zote.Wakati Mwingine tunashindwa kucheza vizuri mikoani kwa kua viwanja vinakua havina ubora mzuri." Yanga imepata ushindi wa Mabao 5-1 dhidi ya Jkt Ruvu na hivyo kuamsha mbio za ubingwa dhidi ya Azam ambao ndio vinara wa ligi hiyo,lakini Juma Kaseja na Mshambuliaji Raia wa Uganda Emmanueli Okwi hawajakuepo kwenye kikosi kilicho anza wala kwenye benchi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni