Jumatano, 9 Aprili 2014

MZUNGU KICHAA AMCHANA ALI KIBA......

Kati ya vitu ambavyo husaidia kuongeza thamani ya Msanii katika macho ya mashabiki ni pamoja na watu kuona akipata dili kubwa na kulipwa pesa nyingi  katika show lakini kumekuwepo baadhi ya wasanii ambao wakati mwingine hutengeneza mazingira ya uongo hasa kupitia mitandao ya kijamii na wengine hata kufanya interview ili tu kufanya watu waamini kuwa thamani yao iko juu.
  Mzungu kichaa yuko tofauti kidogo katika hilo,sababu haoni sababu ya msanii kudanganya kwa kila kitu ambacho sio kweli.Msanii wa Denmark aliyeishi Tanzania kwa miaka mingi alizungumzia swala hilo katika kipindi cha sporah.
  "Mimi siwezi kwenda kwenye vyombo vya habari nakusema ooh nimetengeneza millioni mia kwenye show halafu media zote ziseme 'oooh wow....' kama alivyo fanya Ali Kiba kipindi fulani"alisema mzungu kichaa
"Alisema alikua anataka kwenda kufanya show ujerumani na alikuja kusema ameahirisha kwenda,tena aliahirisha siku moja kabla,na kusema kuwa angelipwa shilingi milioni 100....kwa hiyo akadai kwamba alikua anapewa hiyo hela lakini mikataba haikwenda kama ilivyotakiwa aliahirisha show siku moja kabla na kama Mwanamuziki mimi najua jinsi mambo ambayo hua yanakuwa siamini watu waliokuwa tayari kumlipa kiasi cja pesa kama hicho na kwa wao kutafuta media publicity kupreted we are getting big money to perform nadhani hilo ni kosa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni