Jumapili, 18 Mei 2014

Msanii Adamu Kuambiana afariki dunia

Adamu Kuambiana enzi za uhai wake akiwa location. Mwigizaji na Muongozaji wa filamu hapa nchini ADAMU KUAMBIANA amefariki dunia tarehe 17/05/2014, baada ya kuanguka location. Star mkubwa wa filamu nchini amenitumia ujumbe ulio someka hivi "Msanii Adamu Kuambiana amefariki dunia sasa hivi alikua location kaanguka ghafla,Maiti ipo hospital ya Marrie Stopes,Mwenge Dar es salaam.... hospitali Ambayo Ndugu Adamu Kuambiana amefariki..Marie Stopes.Mwenge Dar es Salaam. Mwenyekit wa Bongo Movie Steve Nyerere amesema "Mwenzetu Adam Philipo Kuambiana amefariki akiwa location akiwa ana shoot movie.Mimi nimepigiwa simu saa3 asubuhi kuwa niende pale hospitali mwenge ni kahakikishe kuwa ni kweli Adamu anefariki na kweli kufika pale nikamkuta Adam kuambiana amefariki.....rais wa bongo movie Steve Nyerere akiwa ktk majozi makubwa.... "Sasa tumetoka Muhimbili kwenda kumstiri Mwenzetu,..."alisema Steve. Taarifa ina sema wakati akiwa location alikua analala mika.tumbo linamuuma linamuuma kumfikisha hospital ndipo umauti ukamfika. Kwa mujibu wa Steve Nyerere amesema marehemu Adamu kuambiana alikua ana shoot filamu yake mpya ambayo ndani yake ali washirikisha wasanii wa bongo fleva akiwemo Q chilah. Taratibu za mazishi na msiba nitawafahamisha kila kinachoendelea.. Mwili wa Aliye kuwa Mwigizaji na Muongozaji wa filamu hapa nchini ADAMU KUAMBIANA ukiwa monchwari katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini dar es salaamu.Mungu ailaze roho ya marehemu Adamu Kuambiana mahala pema peponi Amina. hawa ni baadhi ya Ndugu,wa sanii,wapenzi wa Aliye kuwa msanii wa bongo movie Marehemu Adamu Kuambiana Wakiwa katika majozi ya kumlilia ndugu yet Adamu kuambiana. Mwandishi na mmiliki wa Hancyblog akiwa katika huzuni ya kumkumbuka aliye kuwa Msanii wa Bongo movie ndugu Adamu kuambiana .Bwana Hancy Abdillahi Anawapa pole wa sanii wote,Familiya ya Adam kuambiana Wapenzi wa Adamu na Taifa zima kwa ujumla. Mungu ailaze roho ya marehemu Adamu Kuambiana Mahala pema peponi Amina.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni