Jumapili, 18 Mei 2014

MAZISHI YA MSANII ADAMU KUAMBIANA KUFANYIKA MAKABURI YA KINONDONI

Mazishi Ya muongozaji na Msanii wa filamu ADAMU KUAMBIANA yatafanyika Jumanne (may 20) katika makaburi ya kinondoni jijini dar es salaamu.
  Akizungumza Mwenyekiti wa Bongo movie.STEVE NYERERE amesema kuwa marehemu ataagwa leaders club siku hiyo hiyo kabla ya mazishi.
  "habari za mazishi ni kwamba atazikwa siku ya jumanne na tutazika katika makaburi  ya kinondoni ,kuagwa ataagwa siku hiyo hiyo katika viwanja vya leaders club kuanzia saa 3asubuhi mpaka saa9 na baada ya hapo tutaelekea makaburini alisema steve

Pia Steve Nyerere amedai kuwa marehemu Adamu kuambian alikua na matatizo ya tumbo ambayo ndo yadaiwa kuwa chanzo cha kifo chake "Marehemu alikua anasumbuliwa na vidonda vya tumbo ndivyo kifo chake kilivyotokea Marehemu Adamu kuambiana katika muonekano wake wa mwisho kabla ya mauti kumfika

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni