Jumapili, 18 Mei 2014

MAJANI YA PAPAI HAYATIBU DENGUE........usidanganyike mwananchi.

Halimashauri ya manispaa yao Ilala imesema kuwa majani ya mpapai sio tiba ya Ugonjwa Wa Dengue hivyo ni vyema wananchi wakafika hospitalini kupatiwa dawa kuliko kudanganyika na waganga wa jadi....  
Kauli hiyo ilitolewa Dar es salaam jana na kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala DR.WILLY SANGO, wakati wakitoa mafunzo kwa wenyekiti wa serikali za mitaa jinsi ya kuelimisha wananchi jinsi ya kujikinga na Homa ya Dengue.....
  Dr Sango alisema ugonjwa wa dengue  haunatiba wala chanjo bali wa natibu dalili za ugonjwa huo hata hivyo ni vyema wananchi wakachukua tahadhari ya kujikinga nao.
Pia aliwataka wa ganga wa jadi kuacha kuwadanganya wananchi  kwa kusema kuwa majani ya papai yanatibu kwani hiyo si kweli na hayajathibitishwa na wataalamu wa Afya.....

Alisema kuwa mtu akigundua anatakiwa aende hoapitali kwanza,asiende kutumia dawa bila kupima kwani hiyo nu hatari hivyo wananchi wanatakiwa kufika hospitalini ndipo waanze kutumia dawa. Hata hivyo alisema wenyekiti wa Serikali za mitaa wanatakiwa kuhakikisha wanasimamia vizuri maeneo yao pamoja na kushauri wananchi kwenda hospitali na kuacha kudanganyika na majani ya Mapapai "Majani ya papai si dawa ya dengue wala haijathibitishwa na mpaka sasa hakuna dawa ya ugonjwa huo.Tunatibu dalili zake tu,hivyo wananchi msidanganyike na waganga wachache wanaotaka pesa alisema Dr Sango. Pia alisema kuanzia tarehe 18/5/2014 dawa zitaanza kupuliziwa mtaa mmoja baada ya mwingine ili kuuwa mazalia ya mbu hao wanaoeneza ugonjwa huo........ Hata hivyo alisema kuwa watu wanaopulizia dawa hizo watambuliwe kwanza ndipo waendelee na zoezi hilo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni