Jumanne, 20 Mei 2014

HII NDIO SAFARI YA MWISHO YA MUIGIZAJI NA MUONGOZAJI ADAMU KUMBIANA

Mei 20 saa 9 alasiri ndiyo safari ya mwisho ya Muongozaji na Muigizaji kutoka kiwanda cha.filamu Tanzania Adamu Philip Kuambiana Ambae amepumzika kwenye makaburi ya kinondoni.Mahali alipozikwa Msani Mwenzake STEVEN KANUMBA.
Ujumla wa watu waliojitokeza niwengi sana hasa wasanii wa filamu ambao asilia kubwa wamejitokeza kumzika ADAM KUAMBIANA.

Hizi ni baadhi ya picha za kuanzia leaders wakati wa kutoa heshima za mwisho mpka anazikwa kweny makuburi ya kinondoni

....................................................................

Jumatatu, 19 Mei 2014

MISS RUVUMA AANIKA NYETI HADHARANI...

Miss Ruvuma 2006,Isabela Mpanda amedhihirisha jinsi asivyo jieshimu baada ya kuvua Nguo hadharani na kuacha nyeti zake nje bila kujali watu waliokua wakimshangaa.
  Tukio hilo la kushangaza lilitokea alhamisi iliyopita kwenye ukumbi wa Mawela uliopo sinza,Dar ambako kulikua na kitchen party ya mwigizaji Vanita Omary ambapo Isabela aliwashangaza watu baada ya kuacha nyeti zake nje.

Bila chembe ya aibu Isabela akivalia gauni fupi akiwa tilalila,alikua akicheza muziki huku akinyanyua gauni lake juu na kuacha sehemu nyeti za makalio nje na kusababisha kufuli ya muundo wa bikini kuonekana. Ishu hiyo ilizua mnong'ono kwa baadhi ya wageni waalikwa na kubaki wakimshangaa kwa kitendo hicho. Akiwa anafanya tukio hilo la kujifunua alisikika akisema amepania sherehe hiyo kwani yeye ndiye wifi wa Vanita na kama muigizaji Jackline wolper aliacha kufuli lake kubwa wazi na yeye aliamua kuonesha lake aina ya bikini nje ili lionekane kwani ni la bei kubwa

Jumapili, 18 Mei 2014

MAJANI YA PAPAI HAYATIBU DENGUE........usidanganyike mwananchi.

Halimashauri ya manispaa yao Ilala imesema kuwa majani ya mpapai sio tiba ya Ugonjwa Wa Dengue hivyo ni vyema wananchi wakafika hospitalini kupatiwa dawa kuliko kudanganyika na waganga wa jadi....  
Kauli hiyo ilitolewa Dar es salaam jana na kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala DR.WILLY SANGO, wakati wakitoa mafunzo kwa wenyekiti wa serikali za mitaa jinsi ya kuelimisha wananchi jinsi ya kujikinga na Homa ya Dengue.....
  Dr Sango alisema ugonjwa wa dengue  haunatiba wala chanjo bali wa natibu dalili za ugonjwa huo hata hivyo ni vyema wananchi wakachukua tahadhari ya kujikinga nao.
Pia aliwataka wa ganga wa jadi kuacha kuwadanganya wananchi  kwa kusema kuwa majani ya papai yanatibu kwani hiyo si kweli na hayajathibitishwa na wataalamu wa Afya.....

Alisema kuwa mtu akigundua anatakiwa aende hoapitali kwanza,asiende kutumia dawa bila kupima kwani hiyo nu hatari hivyo wananchi wanatakiwa kufika hospitalini ndipo waanze kutumia dawa. Hata hivyo alisema wenyekiti wa Serikali za mitaa wanatakiwa kuhakikisha wanasimamia vizuri maeneo yao pamoja na kushauri wananchi kwenda hospitali na kuacha kudanganyika na majani ya Mapapai "Majani ya papai si dawa ya dengue wala haijathibitishwa na mpaka sasa hakuna dawa ya ugonjwa huo.Tunatibu dalili zake tu,hivyo wananchi msidanganyike na waganga wachache wanaotaka pesa alisema Dr Sango. Pia alisema kuanzia tarehe 18/5/2014 dawa zitaanza kupuliziwa mtaa mmoja baada ya mwingine ili kuuwa mazalia ya mbu hao wanaoeneza ugonjwa huo........ Hata hivyo alisema kuwa watu wanaopulizia dawa hizo watambuliwe kwanza ndipo waendelee na zoezi hilo

MAZISHI YA MSANII ADAMU KUAMBIANA KUFANYIKA MAKABURI YA KINONDONI

Mazishi Ya muongozaji na Msanii wa filamu ADAMU KUAMBIANA yatafanyika Jumanne (may 20) katika makaburi ya kinondoni jijini dar es salaamu.
  Akizungumza Mwenyekiti wa Bongo movie.STEVE NYERERE amesema kuwa marehemu ataagwa leaders club siku hiyo hiyo kabla ya mazishi.
  "habari za mazishi ni kwamba atazikwa siku ya jumanne na tutazika katika makaburi  ya kinondoni ,kuagwa ataagwa siku hiyo hiyo katika viwanja vya leaders club kuanzia saa 3asubuhi mpaka saa9 na baada ya hapo tutaelekea makaburini alisema steve

Pia Steve Nyerere amedai kuwa marehemu Adamu kuambian alikua na matatizo ya tumbo ambayo ndo yadaiwa kuwa chanzo cha kifo chake "Marehemu alikua anasumbuliwa na vidonda vya tumbo ndivyo kifo chake kilivyotokea Marehemu Adamu kuambiana katika muonekano wake wa mwisho kabla ya mauti kumfika

Msanii Adamu Kuambiana afariki dunia

Adamu Kuambiana enzi za uhai wake akiwa location. Mwigizaji na Muongozaji wa filamu hapa nchini ADAMU KUAMBIANA amefariki dunia tarehe 17/05/2014, baada ya kuanguka location. Star mkubwa wa filamu nchini amenitumia ujumbe ulio someka hivi "Msanii Adamu Kuambiana amefariki dunia sasa hivi alikua location kaanguka ghafla,Maiti ipo hospital ya Marrie Stopes,Mwenge Dar es salaam.... hospitali Ambayo Ndugu Adamu Kuambiana amefariki..Marie Stopes.Mwenge Dar es Salaam. Mwenyekit wa Bongo Movie Steve Nyerere amesema "Mwenzetu Adam Philipo Kuambiana amefariki akiwa location akiwa ana shoot movie.Mimi nimepigiwa simu saa3 asubuhi kuwa niende pale hospitali mwenge ni kahakikishe kuwa ni kweli Adamu anefariki na kweli kufika pale nikamkuta Adam kuambiana amefariki.....rais wa bongo movie Steve Nyerere akiwa ktk majozi makubwa.... "Sasa tumetoka Muhimbili kwenda kumstiri Mwenzetu,..."alisema Steve. Taarifa ina sema wakati akiwa location alikua analala mika.tumbo linamuuma linamuuma kumfikisha hospital ndipo umauti ukamfika. Kwa mujibu wa Steve Nyerere amesema marehemu Adamu kuambiana alikua ana shoot filamu yake mpya ambayo ndani yake ali washirikisha wasanii wa bongo fleva akiwemo Q chilah. Taratibu za mazishi na msiba nitawafahamisha kila kinachoendelea.. Mwili wa Aliye kuwa Mwigizaji na Muongozaji wa filamu hapa nchini ADAMU KUAMBIANA ukiwa monchwari katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini dar es salaamu.Mungu ailaze roho ya marehemu Adamu Kuambiana mahala pema peponi Amina. hawa ni baadhi ya Ndugu,wa sanii,wapenzi wa Aliye kuwa msanii wa bongo movie Marehemu Adamu Kuambiana Wakiwa katika majozi ya kumlilia ndugu yet Adamu kuambiana. Mwandishi na mmiliki wa Hancyblog akiwa katika huzuni ya kumkumbuka aliye kuwa Msanii wa Bongo movie ndugu Adamu kuambiana .Bwana Hancy Abdillahi Anawapa pole wa sanii wote,Familiya ya Adam kuambiana Wapenzi wa Adamu na Taifa zima kwa ujumla. Mungu ailaze roho ya marehemu Adamu Kuambiana Mahala pema peponi Amina.