Jumatano, 27 Novemba 2013

KITALE ATOA YA MOYONI SIKU AKIFA

Muigizaji na mwimbaji nchini Kitale yuko Tanga alipoenda kuhudhuria Dua ya kumuombea marehemu Sharo Milionea ikiwa ni mwaka mmoja tangu afariki dunia kwa ajali mbaya ya gari.

Kitale ambaye ndiye msanii pekee aliye fika tanga siku juzi amesema kuwa amejifunza mambo mengi  katika msiba wa rafiki yake Sharo milionea,Ikiwa ni pamoja na misiba ya wasanii wengine  waliotangulia mbele ya haki Kanumba na Sajuki.

Akiongea kwa njia ya simu na Edson Mkisi katika kipind cha hatua tatu cha 100.5times fm, kitale amesema kutokana na funzo alilo pata amempa ujumbe mama yake ili kwamba pindi atakapo tangulia mbele za haki mambo hayo yasijirudie kwake.

"nimejifunza vitu vyingi na nimejua marafiki walio wema na marafiki wasio wema.Ina maana kwamba kuna marafiki wanafiki na wasio wanafiki .amesema kitale

"kuna vitu vingi ni mejifunza baada ya kuondoka marehemu Steven Kanumba,ni mejifunza baada ya kifo cha Sajuki.Nimejifunza vitu vingi sana sana!:.amesisitiza

"Ina maana hata mimi kama nita tangulia kuna mambo ambayo nimesha mweleza mama yangu na nimesha ieleza familia yangu na fikiri hakitakuja kutokea kama kilicho tokea kwa wenzangu.Nimeji funza vitu vingi hasa ukiwa msanii......kitale aliiambia hatua tatu.
Hata hivyo kitale alikataa kuelezea ujumbe huo na kudai nu siri kati yeye na familia yake kwa kuwa hafahamu nani atatangulia kati yake na Wazazi wake.
Kitale amewashauri wasanii kumkumbuka mungu wakati wanapoendelea na shughuli zao na ndio sababu watu wengi wanaamin kuwa asilimia kubwa ya wasanii ni "FREEMASON',na kwamba hiyo ina tokana na kitendo cha wasanii hao kumsahau Mungu wao.
  Siku kama jana mwaka uliopita (november 27,2012)ndio siku ambayo marehemu Sharo Milionea alizikwa huko Tanga.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni