Alhamisi, 28 Novemba 2013

NORAH AFUNGUKA NA YAKE:ADAI LAANA ALYO WAACHIA RAY NA JOHARI SASA YA FANYA KAZI

Bada ya hivi karibuni staa wa filamu bongo Ruth Suka 'Mainda' kueleza mazito kuhusu Ray, Johari,na Chuchu hans,Msanii mwenzake.Nuru Nasoro,"Nora" nae amefunguka kuwa laana ya walichomfanyia miaka ya Nyuma itawatesa Ray na Johari mpaka kifo chao. Akizungumza na Gpl,Nora alisema Ray na Johari walimfanyia mambo mabaya yalio sababisha kupotea kabisa kwenye sanaa ya filamu hadi alipoibuka upya hivi karibuni. "kinacho wasumbua Ray na Johari ni laana yangu ba kweli nimeamini Mungu analipa hapahapa dunia kwani walinifanyia mambo ya Ajabu,wakanipoteza kabisa kwenye fani,walinifanya ni changanyikiwe wakijua sita pona,lakini sasa hawaelewani tena wakati walikua wanapendana kama pete na kidole". "Nakumbuka zamani nilikua nikishonea nywele nzuri lazima Ray naye akamnunulie Johari kama hizo za kwangu alimtengeneza Johari akawa anaigiza kama mimi na kujifanya yeye ndio mimi mpaka walipo nipoteza kwenye fani. "Namshukuru Mungu nimejikongoja na hatimaye nimerudi tena kwenye sanaa mabata waliyo kuwa wakinifanyia ya mewarudia wenyewe,jamani mwacheni Mungu aitwe Mungu kwani nakesha nikiomba na nina amini maadui zangu wote wataumbuka mchana kweupeeeee." Alisema Nora.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni