Jumapili, 24 Novemba 2013

RAIS KIKWETE ATOA NENO

Rais Jakaya Kikwete amesema wajibu mkubwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi ni kuisemea vizuri,kuihangaikia na kutetea nchi badala ya kushinda kwenye mablogu wa kiponda,kuibeza na kulalamika.Aidha rais Kikwete amesema kuwa kuishi kwa watanzania nje ya nchi kutaonekana jambo la maana zaidi ikiwa watatumia rasilimali na fursa wanazo zipata ugenini kusaidia kubadilisha halu na maisha ya ndugu zao waliobakia Tanzania.

Rais kikwete pua amewaonya Watanzania hao wasije kuchanganyikiwa na kujichanganya wenyewe kwa kuiga tamaduni za kigeni.

Rais Kikwete aliyasema hayo. alipo zungumza na Watanzania waishio nchin Poland.

Aidha Rais Kikwete alisisitiza
"mbona kazi za mangosi mnazifanya vizuri bila kusukumwa,ama kushawishiwa lakini kazi za kusaudia ndugu zenu hamfanyi hata kama ha muwezi kuwasaidia ndugu zenu mnachangia nini nchi yenu"?

mwisho akasema.........
"msiingize mambo ya kigeni kiasi cha kuanza kuchanganyikiwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni