Jumapili, 24 Novemba 2013

MAUWAJI YA KUTISHA YA ZIDI KUTIKISA JIJI

Mwanafunzi aliyehitimu kidato cha4 mwaka huu,Sharifa Abdallah(18) ameuawa kwa kuchomwa kisu cha shingo na mbavuni chumbani kwa mvulana aliyedaiwa kuwa mpenzi wake maeneo ya kimara golani,dar es salaam.

Tukio hilo lilitokea juzi saa 8:30 mchana na baadae mvulana huyo aliyetambuliwa na polisi kwa jina la Abduli Alpha(22)kujisalimisha ktk kituo cha polisi cha stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani cha ubungo.akidai alikua akitaka akitoroka lakini aliona amefanya dhambi kubwa.

Mama mkubwa wa Marehemu,Mwajuma Khamisi alisema Sharifa alimaliza kidato cha nne ktk sekondari ya Uguluni na alikua akisubiria matokeo.

Alisema juzi waliporejea kutoka kazini hawakumkuta nyumbani waliulizia kwa ndugu kutokana na kwamba hakua na tabia ya kutoka nyumbani,lakini hawakufanikiwa kumpata hadi jioni ndipo polisi walipo wataarifu kupatikana kwa mwili wake kamanda wa polisi Wa mkoa wa Kinondoni,Camilius Wambura alisema baada ya kumhoji mtuhumiwa,alisema akifanya hivyo kutokana na wivu wa kimapenzi,kwani alikua na uhusiano na msichana huyo lakin wazazi wa msichana hawakutaka amwoe hvyo kumtaarifu kuwa amepata mchumba mwingine.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni